Stoneface Bombaa is a writer and community organizer at the Mathare Social Justice Centre (MSJC), where he runs the MSJC Kids Club and Art for Social Change. He is also a podcaster over at Until Everyone Is Free, a Sheng’ podcast/radio show about Pio Gama Pinto.
Wathii! Wathii! Wathii! Nikunoma manze kamethoka. Wame come mausiku za 2:00am kubumburusha makeja tena. Hivi ndio ilikua inasound miaka jamo imeland uku Gethare. Uradi ya utiaji bulldozers ka tatu za green za NYS1, ukicheki taya zake ni za chain na vile ilikua inastep kwa makeja za wasee vinoma before mraiya irauke makeja zao ka rwabe zishaonwa kando ilibidi unarauka vile ulidoz ka umehepa juu umesaraundiwa na machines nne. Yani ukilegeza tu kiasi unasondekwa na tunakulose. Mraiya ilikua ijichoche kuchuja bulldozers ni noma. Ile backup bulldozers imepigwa na majenge na majenge wamecome na lorry ka sita na wamejipin michuma, dotono, na yau yau ilibidi wasee walay low.
Gova ilicheza flat design wasee walijaa gas upuz. Ati Gova ilidai kuletea wasee form fiti ya kumake rodi za kuingia mashinani Gethare. So ilibidi wasee wabumburushwe kwa makeja zao ati ndio spaces za kumake rodi zijipe. Ilibidi wasee walegeze juawakua wanadai vurugu na gova. Kuna wasee walidai hii zako nizauduu wakaleta noma na ajab, walidai Gova aitatubeba ufala hii design ikabidi wamepinga demo ingine gwan ajab. Walivusha na kupinga kasheshe. Hizo ndio waliblanda. Magizani za 2:00am wathi waliraushwa na kelele za bulldozer ka nne nazikibomoa keja za wathii bila kujali rada na safety za wasee wamepinga doz—na tena ni magizani, wasee watarieng’ wapi hiyo matime. Pia kuna vile uwezi leta noma ju zimepigwa escort na mangeje ukivusha tuu hizi ndio tunakupoteza. So ilibidi mamokoro, watoi na wazae waspent night zabe keja yako imebomolewa. Bidha most zilikua destroyed aungeokorea chochote.
Gova ilikemba hii ndio time fiti ya kuleta development ya kumake rodi rodi na rodi. Nani Gethare anadai rodi nani akona hami ya kuride ndai kwa hizo rodi za gova Inamake. Magizani kubumburusha famo wakispend manight magizani na kupigwa na ngeve. Zile air tunabreath ni ya usoto. Swali ni eti ukiwa Gethare utastruggle kubuy ndai ama ni hustrugle kubeat “the slavery of poverty” iko mtaani.
Na hii rada yote ya ubumburush ni ati Gova inadai kuleta Uradi Gethare. Uradi! Uradi! Na uradi. Gova ilikemba ni fiti famo ya mraiya ikibumburushwa kwa makeja zao magizani na mali zao zikuedestroy na kupiga kambi inje na ngeve ndio ati ndio Gova ilete uradi maendeleo mara sijui development. Unarada Gova ilidu hii ushiti ya ubumburush ati ndio spaces za kumake rodi ijipe. Uradi yenye itahelp mraiya ako Gethare kufight usofara. Usofara ndio hewa tunabreathe hii Gethare, Mraiya ikona hamu ya kuend poverty cycle imewakumba ka wera, mdifu, waba, na keja ziko decent but Gova inabumburusha keja zao ati rodi ndio the most essential one hii ni uradi ya kutubeba ufala.
1955 hii ndio time ya fao Gethare kububurushwa. Hii mathega Kenya ilikua inaruniwa na gova ya Brito coz ndio ilikua imetucolonize mamiaka mob. So kuna wathi walidai zii, hii riba ya kufinyiliwa na gova ya Brito inafakupigwa stopper wakadai wajiorganise ndio Kenya iget free. Hiyo mjeshii ilikua inajirada ka Mau Mau. Base yao bwaku ya kupinga matiming ilikua Gethare. Inadaisha eti walikua wanazieng’ kumada walami then wanacome kujisunda mtaani Gethare. So gava ya Brito iliona manjege wa kwake wana malizwa. Alafu hiyo kirende wanacome kujisunda mtaani so gova ikatia zii. Mamorning flani ya 1955, wathi wametulia makejani wengine wamepiga doz waliraushwa na sounds za mabulldozers na imepigwa escort na manjege. Makeja zao zilibomolewa kiubad hadi bila wathi kuwaiwa notification za mtaratara za buburush. Ati reason kuu nikuchuja Mau Mau. Wathi wengi walisuffer vinoma adi ka aukua unapiga Geri ya Mau Mau support. Ilibidi Gethare mzima wasee wapige kambi kwa ngeve bila kuwa na rada ya kudu. Noma ni eti wasee walikua masofara ndio ilikua imewakwach juu hizo makeja zilikua za mabati akuna tofauti na vile Gethare kuko kutoka 1955 adi 2021 rada ya environment ni ile ile.
Nadai ukembe hii ubumburush ilihappen Gethare ya 1955. Ndio hii ubumburush hii happen ni nani walido hii ubumburush? Si Mau Mau walibomoa keja za wathii zii. Na si maraiya wa kawaida ati walichochana wakadai wabomoe makeja zao. Na ni nani walikua kwa power hizo magetha! Ni nani? Ni Gova ya Brito ndio ilikua kusema hiyo matime na ni nani alikua na power ya kuoder manjege wapige escort mabulldozers ndio zipinge ubumburush Gethare, ni nani? Si ni Gova. Gova ya Brito ati ilikua inasaka Mau Mau kwa makeja zao Gethare.
Na ninani alidu ubumburush Gethare 2020? Matime mraiya ilikua imelemewa na ngori ya Covid. Matime mraiya ilikua inadai waba na food the most but ikaonelea rodi na sewer line ndio important. Mraiya ikakwara hiyo riba but magizani venye tu kulihappen 1955 escort ya manjenge na bulldozers ndio vile tu bado ili happen 2020. Gova ya brito 1955 ndio ilimake ubumburush Gethare nandio still after Kenya kuwai independent ndio the same way same system Gova hii yetu ndio ilitumia kubumburusha famo za mraiya Masofara Gethare ya 2020. Ubumburush ikihappen hii design kunawathii hunice wakidai hii ndio inaitwa maendeleo, ati development mara uradi. Mara eti acha Gova ifanye miradi ya kuhelp masofara ndio at least Gethare ikae poa. Ni Development kweli famo ikidoz kwa njeve hii ndiyo tunabanju tukidai ni “uradi”? Masofara chenye walikua wanadai vile Covid ililand Kenya sana hapa Gethare tulikua tunadai essential service ka mdifu na waba. Wewe unanice ukisema ni Development Gova ikileta rodi na sewer line hii matime ya pandemic.
Sio kila mraiya inahappen kuserereka na ile rada yenye country inaproduce. Ukikemba rada ya oil ilipatikanaga turu for real si waturu wanaserereka na hiyo natural resources. Rada safi yenye upatikana hapa kenya akuna day ata jamo tushai serereka tukidai tunajimbamba na natural resources yetu. Most ukuwa extracted Hapa kenya na inasanywa na maempires. Ka London na Brito. Usos inachambuliwa pande jamo inazieng kubost economy ya country zingine then tunabanju tukizihita “development country”.
Na hizi ndio imekua ikihappenig adi waleo.
1National Youth Service